IJUE MAANA YA ISHARA YA MSALABA
Ijue
Ishara ya Msalaba✅
Ishara ya Msalaba ni
tendo la mtu kugusa paji la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na
kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'.
Kugusa paji la uso
tuna maana kukubali kwa akili, kugusa kifua maana yake ni kupokea na kuupenda
msalaba moyoni na kugusa Mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba Msalaba kwa
nguvu zetu zote.
Tunafanya njia ya
Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu Mmoja katika Nafsi tatu. Pia Msalaba ni Ishara
ya Ukombozi wetu.
Ishara ya Msalaba Juu
ya Paji la uso, mdomo na kifua kabla ya injili:
Hii ina maana kwamba
Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu Kwa Akili yangu,
Nitalitangaza kishujaa
kwa midomo yangu, na Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu Wote.
Tumsifu Yesu Kristu, ama hakika website hii ni msaada mkubwa sana kwa wakristo wakatoliki wote, kuanzia walio katika mafundisho ya katekismu katoliki kwaajili ya sakramenti mbalimbali pamoja na wale wenye lengo la kuijenga imani yao vyema.
ReplyDeleteLakini pia Website hii ni msaada mkubwa kwa wale wanaokutana na changamoto za wanaolipiga vita kanisa katoliki.
Sababu kuu inayoifanya website hii kuwa bora zaidi ni kwamba "Website hii ni nyepesi na rahisi sana kuitumia"
Ama hakika Mungu awabariki sana waasisi wa website hii na kuwajalia Roho Mtakatifu ili muendelee kuweka mambo muhimu mengine yaliyosalia.
Bwana awe nanyi nyoteeeee.
"Amen"