IKIMBIE ZINAA KAMA UNAVYOUTOA MGUU WAKO UKIGUSA MOTO
TUJIKUMBUSHE KWA NINI MUNGU ALIANGAMIZA SODOMA NA GOMORA PIA KWA NINI ALILETA GHARIKA KATIKA ARDHI YA NUHU?
Ni vizuri ukumbuke ya kuwa
gharika ilitokea wakati wa Nuhu kwa sababu ya zinaa. “Ikawa wanadamu
walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliona hao binti za
wanadamu – ni wazuri; WAKAJITWALIA WAKE WO WOTE WALIOWACHAGUA. Bwana akasema, ROHO YANGU
HAITASHINDANA NA MWANADAMU MILELE, kwa kuwa yeye ni nyama; basi siku zake zitakuwa mia na ishirini.
Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile, tena baada ya hayo, wana wa Mungu WALIPOINGIA kwa binti za
wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. BWANA AKAONA
YA KUWA MAOVU YA MWANADAMU NI MAKUBWA DUNIANI NA KWAMBA KILA KUSUDI ANALOWAZA MOYONI
MWAKE NI BAYA TU SIKU ZOTE. BWANA AKAGHAIRI KWA KUWA AMEMFANYA MWANADAMU DUNIANI,
AKAHUZUNIKA MOYONI. Bwana akasema, Nitamfutilia usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambulisho
na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa
Bwana.” (Mwanzo 6:1-8)
Ukiendelea kufuatilia habari hii katika Biblia utaona ya kuwa baada ya gharika ya maji walibaki watu nane tu!
Wanadamu wengine wote waliangamia kwa sababu ya nini? – Zinaa! Sodoma na Gomora Wasomaji wa Biblia
wanafahamu kabisa ya kuwa miji ya Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu
kwa sababu ya uasherati uliokuwa ukifanyika ndani yake. Soma Mwanzo 19:4-25. Na pia katika kitabu cha Yuda
1:7 tunasoma hivi: - “Kama vile Sodoma na Gomara, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata UASHERATI kwa
jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa
katika moto wa milele.”
Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani kinamfanya mwanadamu wa siku hizi
adhani ya kuwa Mungu amebadilika juu ya kuadhibu wale wote wafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni
watu watatu tu waliobaki – Lutu na watoto wake wawili! Wanadamu wengine waliokuwa katika miji hiyo
waliteketezwa kwa sababu ya nini – Zinaa! Kuhani Eli na watoto wake. “Basi Eli alikuwa mzee sana, naye alisikia
habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi WALIVYOLALA NA WANAWAKE
waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania.” (1Samweli 2:22)
Hata baada ya baba yao kuwaonya hawakusikia, na matokeo yake ni:-
1. Watoto hao wawili, Hofni na Finehasi walikufa wote siku moja;
2. Wana wa Israeli walipigwa na adui zao Wafilisti na Sanduku la agano likatekwa;
3. Kuhani Eli alikufa.
Yote haya yalitokea katika taifa ambamo watoto wawili wa kiongozi waliuwa wakifanya mambo ya Zinaa bila
hata kujali maonyo. Je! Bado unajiuliza kwa nini nilitoa machozi baada ya kusikia sauti ya Mungu katika ndoto
ikisema “Nitachukuliana mpaka lini na mwanadamu afanyaye mambo ya jinsi hiyo?” Siku za Mwisho. “Lakini
ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye
kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao,
wasio na shukrani, wasio safi…….Kwa maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU,
NA KUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI, waliochukuliwa na tamaa za
namna nyingi. (2 Timotheo 3:1,26).
Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo ya zinaa? Vishawishi vimekuwa vingi,
na wanawake wengi wameanguka katika mitego hiyo ya kupenda fedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya
uzinifu. Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimewapofusha macho wasione
ya kuwa uzinifu ni mbaya?
Biblia inasema; “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi yake.”
(Mithali 6:32) Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na nataka
nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo ndani yako na kuliona jambo hili jinsi linavyomhunish
Mungu, hakika hutatulia; na hapana budi macho yako yatajaa machozi juu ya kizazi hiki kinachojiangamiza
chenyewe kwa sababu ya zinaa.
Sababu ya mambo haya kuandikwa. Mambo haya hayakuandikwa kwa bahati mbaya, wala si kwa ajili ya
kuonyesha historia ya watu Fulani tu. Bali yaliandikwa kwa kusudi maalumu na muhimu. “Basi mambo hayo
yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili KUTUONYA SISI, tuliofikiriwa na miisho ya zamnai – Kwa
hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” (1 Wakorintho 10:11,12)
Na mimi nimependa kuyaonyesha wazi ili tujue tunapozungumza juu ya zinaa, Bwana Mungu anakuwa na
mawazo gani juu yake. Nafahamu si mara kwa mara hata katika mahubiri na mafundisho, jambo hili huguswa
kwa undani. Lakini naona umefika muda wa kulichambua jambo hili kwa undani zaidi. Hali ilivyo sasa. Mtu mmoja
aliniuliza “Je, mtu aliyeokoka anaweza kufanya mambo ya uasherati – je, anaweza kuzini?” Nikamwambia, “Mtu
aliyeokoka hatakiwi kufanya mambo ya uasherati, kwa kuwa kufanya hivyo ni dhambi, lakini asiposimama katika
Kristo sawasawa anaweza kuzini.” Halafu huyo mtu akaendelea kuuliza, “Je, Unamfahamu Fulani? (Akamtaja jina
lake). “Ndiyo namfahamu.” Mimi nilimjibu, na nikaendelea kusema; - “ kuwa ni mtumishi wa Mungu, ingawa
sijamwona muda mrefu umepita sasa”. Ndipo akasema, “Unafahamu ya kuwa alianguka na akazini na msichana
Fulani (akamtaja jina lake) ambaye pia ameokoka, na sasa yule msichana amezaa?” Mimi nilishangaa na
kushutushwa na habari hizo. Nikamuuliza “Unasema kweli ndivyo ilivyotokea?” Akasema, “Ndiyo” Ndipo Roho
wa Mungu aliponikumbusha ndoto ile aliyonipa. Katika ujumbe ule wa ndoto, Mungu alinionyesha mkristo
aliyeokoka akifanya mambo ya uasherati. Kwa mtu asiyeokoka siwezi kushangaa akifanya uzinzi, kwa kuwa bado
yuko gizani, na yuko chini ya mkuu wa giza, ibilisi – kwa hiyo anaweza kufanya lo lote lile.
Ndiyo maana mtu anaweza kusema yeye ni mkristo, na huku anazini mara kwa mara. Mkristo wa kweli
aliyeokoka hatakiwi kuzini, wala kushindwa na dhambi. Kwa nini? Kwa kuwa ndani yake ametengwa mbali na
dhambi, na amepewa ushindi juu ya dhambi. Ushindi dhidi ya dhambi Uhusiano wako na dhambi unakuwaje
baada ya kuokoka, na kufanyika kiumbe kipya ndani ya Kristo? Watu wengi wakiisha-okoka, huwa bado
wanasumbuliwa na kuanguka katika dhambi mara kwa mara, na hasa katika zinaa. Na hii inatokea kwa kuwa
hawapati mafundisho ya kutosha ya neno la Mungu juu ya jinsi wanavyotakiwa kuenenda katika maisha mapya
waliyopita. Kaini aliambiwaje na Mungu? Bwana alimwambia hivi; “ kama ukitenda vyema, hutapata kibali?
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa UISHINDE”
(Mwanzo 4:7)
Na ndivyo ilivyo hata sasa. Bado tumo ulimwenguni humu, ingawa aliyezaliwa mara ya pili yeye si wa ulimwengu
huu (Yohana 17:16). Lakini kwa kuwa bado tumo katika ulimwengu uliojaa dhambi inayotutamani kila siku, na
tusije tukajisahau. Inatupasa tuishinde. Yanenaje maandiko? Imeandikwa katika kitabu cha (Warumi 6:12-14)
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee
kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai
baada ya kufa, na viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama
walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana DHAMBI HAITA
WATAWALA NINYI, kwa sababu hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema”. Ikiwa tunaambiwa ya kuwa
“Dhambi haitawala ninyi …….” inakuwaje basi wengine wanatawaliwa nayo? Inakuwaje mtu wa Mungu,
aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu aanguke katika zinaa? Kitu gani kinampofusha macho ya rohoni? Je! Ni
halali kwa mtu anayekaa ndani ya Kristo kutenda dhambi? Yanenaje maandiko? “Kila akaaye ndani yake (Yesu
Kristo) HATENDI DHAMBI; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtamua….atendaye dhambi ni wa
ibilisi; kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili
azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:6,8) Je! Unaona maneno haya yalivyoandikwa kwa ajili yetu? Sidhani kama
unapenda tena kuwa Ibilisi kwa kuwa “Apendaye dhambi ni wa Ibilisi” Kwa hiyo ni muhimu ujilinde usitende
dhambi. Tena imeandikwa: “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu UZAO WAKE WAKAA
NDANI YAKE; WALA HAWEZI KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU.” (1 Yohana
3:9) Ikiwa umezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, ujue hakika UZAO WA MUNGU unakaa n dani yako. Na
uzao huu wa uungu ni Mtakatifu, na unakaa ndani yake bila kutangatanga unakuwezesha kuishi bila kutenda
dhambi.
Je! Si jambo la kumshukuru Mungu hilo. Si kwamba anatuambia tusitende dhambi bila kutupa njia ya kutusaidia.
Anajua sisi wenyewe hatuwezi kuishinda dhambi, BALI YEYE AKIKAA NDANI YETU NA SISI NDANI YAKE
TUNAWEZA KUISHI KATIKA USHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MITEGO YAKE YOTE. Tena imeandikwa; “Twajua ya
kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu HATENDI DHAMBI; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJI LINDA, wala yule
mwovu HAMGUSI.” (1 Yohana 5:18) Ee, mtu wa Mungu, jilinde basi kwa kuwa umezaliwa na Mungu, kwa nini
tamaa ya uasherati ikusonge? Je?! umesahau ni uzao wa namna gani ulio ndani yako? Ni kweli kwamba mtu
akitenda dhambi na akatubu, Bwana atamsamehe, (1 Yohana 1:9). Lakini hatutakiwi kutenda dhambi. Ndiyo
maana imeandika; “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba MSITENDE DHAMBI”…. (1 Yohana 2:1)
Sasa naona unaweza kuelewa kwa nini inashtusha na kusikitisha unaposikia mtu wa Mungu ameanguka katika
dhambi ya zinaa.
Ikiwa maisha ya wokovu yatakuwa ni ya kuanguka na kusimama, halafu tena kuanguka na kusimama mara kwa
mara; basi ina maana ya kuwa ushindi wa kutosha haukupatikana pale msalabani. Lakini nataka nikuambie hivi,
ushindi kamili ulipatikana pale msalabani bila kubakiza kitu! Ndiyo sababu Yesu Kristo alikuwa na ujasiri wa
kusema ‘IMEKWISHA’ pale msalabani. Tunachotakiwa kufanya ni kuwa watendaji wa neno; na ndiyo ushindi huo
utadhihirika katika maisha yetu. Usidhani ya kuwa mapokeo ya wanadamu yanaweza kukusaidia kuishinda
dhambi; la hasha! Yesu Kristo peke yake akikaa ndani ya moyo wako, na neno lake ukilitii, ndiko utapata ushindi
halisi na halali dhidi ya dhambi. Swali la kujiuliza Idadi ya wakristo waliookoka wanaoanguka katika dhambi ya
zinaa inaongezeka siku baada ya siku. Na wengine wameanguka dhambini moja kwa moja, hata haja ya kutaka
kusimama upya katika Bwana imepotea. Wanaona aibu! Na wengine wanaanguka na kusimama, halafu tena
wanaanguka na kusimama.
Na kwa sababu hiyo hawana ushuhuda mzuri mbele za watu. Hawaaminiki tena. Lakini je! Unadhani Mungu
atatuambia tuishinde dhambi wakati anafahamu ya kuwa hatuna uwezo huo? La hasha! Mungu wetu
tunayemwamini katika Kristo Yesu si dhalimu kiasi hicho. Jambo ninalofahamu ni kwamba ametuambia tuishinde
dhambi kwa kuwa ndani yetu sisi tuliompokea, ametupa UWEZA WA KUISHINDA DHAMBI – kwa namna gani?
“Kwa sababu UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE (YETU) WALA HAWEZI (HATUWEZI) KUTENDA DHAMBI KWA
SABABU AMEZALIWA (TUMEZALIWA) KUTOKANA NA MUNGU”.(1Yohana 3:9) Uzao wako si uzao wa kuanguka
dhambini, bali ni uzao wa kushinda dhambi, kwa kuwa Kristo anakaa ndani yako!

Post Comment
No comments